HabariMilele FmSwahili

Paketi 1 ya kilo 2 ya unga wa ugali kuuzwa shilingi 75 kuanzia leo

Paketi moja ya kilo 2 ya unga wa ugali itauzwa shilingi 75 kuanzia leo. Ndilo agizo la waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri ambaye amewataka wafanyabiashara  kutekeleza bei hiyo mara moja.Kiunjuri anasema bei hiyo imechangiwa  na makubaliano kati ya serikali na wasanga nafaka nchini ambao mapema juma hili waliondoa hofu ya kuathirika na ushuru wa  asilimia 8 unaotozwa bidhaa za mafuta .Aidha Kiunjuri amedokeza shilingi bilioni 1.4 zimetolewa na serikali kupunguza deni wanalodaiwa na wakulima wa mahindi nchini

Show More

Related Articles