HabariMilele FmSwahili

Polisi wawakamata washukiwa 9 wa machafuko Olepusimoru

Polisi kaunti ya Narok wanawazuilia washukiwa 9 wanaohusishwa na machafuko yalioshuhudiwa eneo la Olposemoru. 9 hao waliokamatwa jana usiku watafikishwa mahakamani alasiri hii. Kamishna wa Narok George Natembeya anasema 9 hao walinaswa wakiwa wamebeba  mishale 126, panga na rungu. Tayari maeneo kuna marufuku ya kutotoka nje, kati ya saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi eneo hilo la Olposimoru

Show More

Related Articles