HabariMilele FmSwahili

Oyamo kusalia rumande hadi tarehe 8 Oktoba

Micheal Oyamo msaidizi wa gavana wa Migori Okoth Obado atasalia mikononi mwa polisi hadi Oktoba nane.Jaji wa mahakama kuu Jessi Lessit anasema Oyamo anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji ya Sharon Otieno atasalia rumande hadi jumatatu ya Octoba nane ambapo atabaini iwapo ataachiliwa huru kwa dhamana au la.Awali Oyamo alikanusha mashtaka hayo ya mauaji huku mawakili wake wakiitaka mahakama kumpa dhamana.Oyamo,gavana Obado pamoja na watu wengine 6 wanakabiliwa na kesi hiyo ya mauaji ya Sharon huku Obado akisubiri kesho mchana kubaini iwapo ataachiliwa kwa dhamana au la.

Show More

Related Articles