HabariPilipili FmPilipili FM News

Tahadhari Ya Mvua Kubwa Yatolewa Katika Kanda Ya Pwani.

Idara ya hali ya hewa nchini imetoa onyo la mvua nyingi kunyesha katika kanda ya Pwani kuanzia hii leo.

Kulingana na mtaalamu wa maswala ya hali ya hewa, kanda ya pwani itapokea mvua ya zaidi ya milimita 30 ndani ya masaa 24 na itaambatana na upepo mkali na mawimbi makubwa.

Ifikapo kesho, mvua ya zaidi ya milimita 50 inatarajiwa lakini kiwango hiki kinatarajiwa kipungue hadi milimita 30 siku ya ijumaa.

Kaunti ambazo zinaweza kuathirika ni pamoja na Kwale, Mombasa, Kilifi, Taita Taveta, Lamu na Tana River. Wakazi wa maeneo haya wanashauriwa kuwa waangalifu kwani mafuriko yanatarajiwa.

Show More

Related Articles