HabariMilele FmSwahili

Msaidizi wa Obado,Michael Oyamo akanusha mashtaka ya mauaji ya Sharon

Msaidizi wa gavana wa Migori Michael Oyamo amekanusha mashtaka ya mauaji ya Sharon Otieno. Upande wa mashtaka umetaka Oyamo aendelee kuzuiliwa kwa muda zaidi, ombi mawakili wa Oyamo wakiongozwa na David Amolo wamepinga.Jaji Jessie Lessit sasa anasubiriwa kutoa uamuzi wake saa sita mchana wa leo iwapo Oyamo atazuiliwa zaidi au ataachiliwa kwa dhamana. Oyamo ambaye ni mmoja wa washukiwa wakuu wa mauaji hayo, amekuwa kizuizini kwa siku 14 sasa.

Show More

Related Articles