HabariMilele FmSwahili

Gavana Mutua aiomba mahakama kuridhia ushindi wake

Gavana wa Machakos Dr.Alfred mutua ameiomba mahakama ya juu kuridhia ushindi wake. Mutua kupitia wakili Kioko Kilokumi anasema kukosa kusainiwa fomu 37b wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana hakuwezi kupelekea yeye kupokonywa ushindi ilivyofanya mahakama ya rufaa. Ameiambia mahakama hiyo chini ya uongozi wa jaji mkuu David Maraga kwamba fomu 37a zilisainiwa na wagombea wote katika vituo vya kupigia kura na haikuwa lazima fomu 37b kusainiwa kabla ya matokeo kujumlishwa katika fomu 37c.

Show More

Related Articles