HabariPilipili FmPilipili FM News

Wawakilishi Wadi Wa Migori Wataka Kumtimua Gavana Obado.

Wawakilishi wadi wa kaunti ya Migori wameanzisha mchakato wa kumtimua mamlakani gavana wa kaunti hiyo Okoth Obado ambaye ameshtakiwa kwa mauaji ya Sharon Otieno.

Kufikia saa kumi na mbili jana jiobi, wawakilishi wadi 23 kati ya 60 wa bunge la kaunti hiyo walikuwa wametia saini hoja ya kumbandua Obado kwa misingi ya ukosefu wa maadili.

Hata hivyo kinara wa wengi bungeni humo amepuzilia mbali shinikizo hizo.

Show More

Related Articles