HabariMilele FmSwahili

Mama amnyonyesha na kumuambukiza mtoto virusi vya HIV Nakuru

Mwanamke wa miaka 29 ameshtakiwa katika mahakama ya nakuru kwa madai ya kumnyonyesha na kumuambukiza virusi vya HIV mtoto wa jirani yake. Susan Njeri akifika mbele ya hakimu mkuu Joe Omido hata hivyo amekanusha mashtaka ya kumuambukiza HIV mtoto huyo wa miezi 9. Hakimu Omido aidha amekosa kumuachilia kwa dhamama mshukiwa na badala yake kuagiza azuiliwe katika kituo cha polisi cha Njoro. Hakimu huyo pia ameagiza mshukiwa afikishwe mbele yake tena Oktoba 2 akiwa ameambatana na ripoti ya uchunguzi wa afya sawa na ya mtoto husika.

Show More

Related Articles