HabariMilele FmSwahili

Mwili wa msichana wa miaka 16 wapatikana ndani ya mto Meru

Mwili wa msichana wa miaka 16 umepatikana katika mto wa Majau maeneo ya Gakoromone, Meru.Inadaiwa msichana huyo alidhulumiwa kimapenzi kabla ya kuuawa. Wakaazi wanadai tukio silo la kwanza kwani kumekuwa na ongezeko la utovu wa usalama eneo hilo.Aidha chifu wa eneo hilo Starnley Ngeera anasema visa vingi vimeripotiwa maeneo hayo na hakuna mshukiwa hata mmoja amewahi kutiwa mbaroni.

Show More

Related Articles