HabariPilipili FmPilipili FM News

Mbunge Wa Kisauni Ali Mbogo Ayasuta Mashirika Ya Kijamii Katika Eneo La Pwani.

Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo ameyakemea vikali mashirika ya kijamii kwa kile anachokitaja nikukosa uwazi  na niasafi wakati wa kuendesha majukumu yake.

Akiongea kwenye mahojiano yetu, Mbogo anasema mashirika ya kijamii yamekuwa yakifumbia macho visa vya uhalifu  vinavyotekeleza na magenge ya wahalifu  lakini badaye huandamana pale wahalifu wanapokabiliwa na serikali.

Mbogo sasa anayataka  mashirika ya HAKI AFRICA na MUHURI  kueleza wazi wazi nia yake katika jamii, ya ni haki ya nani wanayoitetea.

Aidha pia mbogo amewataka wazazi kuwashauri vyema watoto wao na kuwa yeye kama mbunge.

Show More

Related Articles