HabariPilipili FmPilipili FM News

IEBC Yakanusha Kumfuta Kazi Chiloba.

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imekanusha taarifa za kufutwa kazi kwa Ezra Chiloba.

Hii ni baada ya taarifa za habari kuashiria kuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amemfuta kazi Chiloba kufuatia utumizi mbaya wa pesa wakati wa uchaguzi mkuu wa 2017.

Duru ziliarifu kuwa uamuzi wa kumfuta kazi Chiloba uliafikiwa katika mkutano uliofanywa baina ya Chebukati na makamishna Boya Molu na Abdi Guliye.

Show More

Related Articles