HabariMilele FmSwahili

KDF Yawauwa magaidi 10 wa Alshabaab kaunti ya Lamu

Wapiganaji 10 wa kundi la kigaidi la Alshabab wameuwawa kufuatia shambulizi lililotekelezwa na jeshi la KDF kwenye kambi yao huko Pandanguo kaunti ya Lamu. Katika taarifa afisa wa mawasiliano wa KDF Paul Njuguna  anasema vikosi vya KDF vilishambulia kambi ya Al shabab katika eneo la Taksile kaskazini mwa Pandanguo saa moja kasorobo asubuhi hii. Amedhibitisha kuwa bunduki 7 aina ya AK 47 na risasi kadhaa zilinaswa. Wanajeshi 3 wa KDF walijeruhiwa. Njuguna anasema wanajeshi wanawasaka wapiganaji wengine waliotoroka.

Show More

Related Articles