HabariPilipili FmPilipili FM News

Eneo La Jomvu La Vamiwa Na Funza Na Kunguni.

Wakaazi wa Jomvu kaunti ya Mombasa wanahangaishwa na wadudu Funza na Kunguni hali iliyotajwa kufanya watoto wengi kushindwa kwenda shuleni.

Mwenyekiti wa kikundi cha MIJARI kinachojishugulisha na kutoa matibabu kwa waathiriwa Ali Kadzora,  amesema hali ni mbaya mno katika sehemu za Chamunyu,Vikobani miongoni mwa maeneo mengine.

Aidha Saumu Ramadhan mmoja wa wana kikundi anasema wazazi wengi wanashindwa kutekeleza majukumu yao kutokana na mahangaiko ya kushambuliwa na Funza na Kunguni.

Show More

Related Articles