HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta akutana na viongozi mashuhuri wa kibiashara Marekani

Rais Uhuru Kenyatta amekutana na kufanya mashauriano na viongozi mashuhuri wa kibiashara nchini Marekani katika dhifa ya chakula cha jioni iliyoandaliwa jijini New York na shirika la ndege la Kenya Airways. Hafla hii imeandaliwa jana kupanga maandalizi ya ziara za moja kwa moja za ndege za Kenya Airways kutoka Kenya hadi Marekani Oktoba 28. Rais Kenyatta aliye Marekani kuhudhuria kongamano la umoja wa mataifa ameipongeza Kenya aAirways na washirika wake kwa kufanikisha azma ya safari hizo. Rais pia amewahimiza wakenya wanaoishi Marekani kutumia fursa hiyo kuwekeza zaidi humu nchini.

Show More

Related Articles