HabariPilipili FmPilipili FM News

Wavuvi Walalamikia Uchafuzi Wa Bahari Katika Eneo La Kibarani.

Wavuvi katika mtaa wa tudor shimanzi wakishirikiana na shirika la kutetea haki za binadamu la HAKI AFRIKA wametoa lalama zao wakidai kwamba kuna baadhi ya kampuni na mabwenyenye bado wanamwaga taka katika eneo la kibarani hata licha ya marufuku kutolewa na serikali ya kaunti.

Wavuvi hao wanasema uchafu huo ambao unaendelea kutupwa kando ya bahari  umefanya samaki wengi kufa na sasa samaki wanaopatikana ni wachache sana.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la HAKI AFRICA hapa Mombasa Hussein khalid  amesema anahofia samaki ambao wanavuliwa sehemu hiyo si salama kwa matumizi ya binadamu.

Show More

Related Articles