English VideosK24 TvNEWSVideos

Gavana wa Migori, Obado anazuiliwa na polisi na anatarajiwa kuwasilishwa mahakamani Jumatatu

Gavana wa Migori Okoth Obado anaendelea kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Gigiri, jijini Nairobi katika uchunguzi wa kubainisha iwapo alihusika na mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo, Sharon Otieno.

Gavana Obado akisuburi kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu ambapo  atafunguliwa mashtaka ya mauaji, inabainika kwamba amesusia chakula au kinywaji korokoroni na kusisitiza kwamba atakula tu chakula kilichotayarishwa na mkewe.

Makachero wamebaini kuwa Gavana huyo, ambaye ni mmoja wa washukiwa wakuu kwa mauaji hayo, alikuwa akiwasiliana na mwendazake msaidizi wake Michael Oyamo, msaidizi wake wa zamani Caspal Obiero, pamoja na  mhudumu  wa texi Jack Gombe, siku ambayo Sharon aliuawa kinyama na kumweka kwenye msururu wa washukiwa wakuu katika  mauaji ya Sharon, huku polisi wakitarajiwa kukamata  washukiwa wengine.

Show More

Related Articles