English VideosK24 TvNEWSVideos

Buriani Marybel Kapolon: Marybel alitekwa nyara na kuuawa Meru azikwa Uasin Gishu

Biwi la simanzi lilitanda katika kijiji cha Ng’nyilel, eneo bunge la Turbo katika mazishi ya mwanae hakimu mkaazi wa Githongo, Caroline Kemei yaliyofanyika Jumamosi na kuhudhuuriwa na maelefu ya waombolezaji.

Kifo cha Marybel kimewashtua Wakenya wengi, huku wanafamilia wakitaka waliohusika kuchukuliwa hatua kali

Mwendazake Marybel Kapolon, aliyekua mwanafunzi wa darasa la nne, shule ya Consolata katika eneo la Imenti Kaskazini, aliripotiwa kutoweka tarehe 6 September kabla ya mwili wake kupatikana msituni Gitoro, kaunti ya Meru akiwa amuewawa , siku chache baada ya kuripotiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana.

Viongozi wa ngazi za juu katika idara ya mahakama, viongozi wa kisiasa na wale wa kidini wote kwa kauli moja wakitaka kitendawili kinachozingira mauaji  hayo tata  kuteguliwa na asasi husika za serikali.

Show More

Related Articles