HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwanafunzi Atandikwa Na Mwalimu Hadi Kufariki.

Mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi ya Mnagoni eneo la Bamba kaunti ndogo ya Ganze amepigwa na mwalimu wake hadi kufariki.

Mwanafunzi huyo kwa jina Mohamed Juma anadaiwa kuadhibiwa pamoja na wenzake mnamo alhamisi juma lililopita lakini baadaye akaanza kulalamikia maumivu mwilini.

Akithibitisha kisa hicho naibu wa chifu katika eneo hilo Japhet Kalama amesema mwanafunzi huyo aliadhibiwa na kuumizwa lakini hakuwaarifu wazazi wake ndipo siku ya jumapili akapelekwa katika hospitali ya Bamba ambapo alipigwa picha na kufanyiwa uchunguzi.

Kulingana na naibu chifu huyo mwanafunzi huyo alionekana na majeraha mabegani sawia na sehemu zengine za mwili wake.

Kwa sasa maafisa wa polisi eneo la Ganze wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho huku juhudi zetu za kuongea na usimamizi wa shule hiyo zikiambulia patupu

Show More

Related Articles