Mediamax Network Limited

Wahudumu Wa Matatu Katika Eneo La Mikindani Wasitisha Mgomo.

Shughuli za uchukuzi wa abiria eneo la mikindani hapa mombasa, sasa zimerejelea  hali yake ya kawaida kuanzia hivi leo asubuhi.

Wahudumu wa matatu eneo hilo, wanasema wamesitisha mgomo wao uliodumu kwa takriban siku 5, baada ya kuafikiana na maafisa wa kaunti na kupewa KITUO chao cha kubebea abiria eneo la Mwembe tayari.

Kwa upande wake mwakilishi wa Wadi ya mikindani Juma Renson Thoya, amewaomba radhi wakaazi wa mikindani kutokana na mahangaiko waliopitia wakati wa mgomo, na kuahidi huduma bora kutokana na mikakati mipya wanayoweka.

Haya yamejiri siku nne baada ya wahudumu wa sekta ya matatu kugoma eneo la mikindani wakilalamikia kuhangaishwa na maafisa wa trafiki eneo la KFA hapa  mjini mombasa.