HabariMilele FmSwahili

Rais atia saini mswada wa fedha wa 2018/2019

Wakenya wataanza kutozwa ushuru wa asilimia 8 kwa bidhaa za mafuta mafuta baada ya rais Uhuru Kenyatta kutia saini sheria ya fedha ya mwaka 2018. Hii ni baada ya bunge kupasisha mswada wa sheriia hiyo jana. Rais Uhuru Kenyatta ameapa kuhakikisha matumizi bora ya fedha zitakazokusanywa kutokana na ushuru huo. Rais ametia saini sheria hiyo  kwenye ikulu ya Nairobi katika hafla iliyoshuhudiwa na naibu wake William Ruto, kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale waziri wa fedha Henry Rotich miongoni mwa viongozi wengine

Show More

Related Articles