HabariPilipili FmPilipili FM News

Idadi Ya Waliofariki Katika Mkasa Wa Ferry Tanzania Yaongezeka.

Miili ya watu 44 imeopolewa kutoka Ziwa Victoria baada ya ferry  iliyokuwa imebeba mamia ya abiria kuzama jijini Mwanza Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe,Kanali Lucas Magembe amesema waliokolewa wakiwa salama ni watu 37, ambapo 32 katia yao wako hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Juhudi za uokoaji bado zinaendelea katika kivuko hicho.

Show More

Related Articles