HabariSwahili

Makachero wanasa Heroin ya kilo 92 ya Sh 300M, Kikambala,Kilifi 

Maafisa wa polisi wa kupambana na matumizi ya mihadarati na dawa za kulevya kwa ushirikiano na maafisa wa idara ya upelelezi wamenasa zaidi ya kilo 92 za dawa ya kulevya aina ya heroine inayokisiwa kuwa ya thamani ya shilingi milioni 300.

Dawa hiyo ya kulevya ilipatikana kufuatia msako katika nyumba moja katika kijiji cha Kikambala kaunti ya Kilifi inayoaminika kumilikiwa na mshukiwa mkuu wa ulanguzi wa dawa za kulevya.

Show More

Related Articles