HabariPilipili FmPilipili FM News

Wahudumu Wa Matatu Watakiwa Kuwa Watulivu.

Wahudumu wa matatu katika wadi ya Mikindani , Jomvu hapa Mombasa wametakiwa kuzingatia amani na usalama eneo hilo, baada ya tofauti kuibuka kuhusu steji wanayopaswa kubebea abiria eneo la KFA.

Akiongea muda mfupi baada ya kukamatwa na kisha kuachiliwa na polisi hapo jana jioni, mwakilishi wa wadi hiyo Juma Renson Thoya amewataka wahudumu wa matatu kusalia watulivu, akisema tatizo lililopo litapata uvumbuzi kuona kuwa wanapata mahali maalum pa kubebea abiria.

Show More

Related Articles