HabariPilipili FmPilipili FM News

Heroine Yanaswa Kilifi

Maafisa wa Polisi kaunti ya Kilifi  wamefanikiwa kunasa kilo 92 za dawa za kulevya aina ya Heroine inayokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 150.

Dawa hizo zimenaswa katika nyumba moja eneo la Kikambala katika kaunti hiyo, katika oparesheni iliyoendeshwa na polisi kwa ushirikiano na maafisa wa kupambana na dawa za kulevya.

Kwa sasa polisi wanaendelea na uchunguzi kuwasaka washukiwa , ikifahamika kuwa wakati wa oparesheni hiyo wenye nyumba hawakuwepo.

Show More

Related Articles