HabariPilipili FmPilipili FM News
Wakaazi Wa Kwale Kunufaika Na Mradi Wa Upanzi Wa Migomba.

Serikali ya kaunti ya Kwale imeanzisha zoezi la kupeana miche ya migomba iliyoboreshwa kwa wakulima ili kufanikisha kilimo biashara .
Akizungumza katika warsha ya kupeana miche hiyo huko ukunda naibu gavana wa Kwale Fatuma Achani amewataka wakulima kuchukulia mradi huo kwa uzito , kwani serikali ya kaunti inapania kujenga soko katika eneo la kombani kuwawezesha kuuza bidhaa zao pale wanapovuna.
Tayari Wakulima 150 kutoka wadi ya ukunda wamenufaika na miche hiyo.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,