HabariMilele FmSwahili

ODM yawataka wabunge wake 2 kufika mbele ya kamati ya nidhamu ya chama hicho

Chama cha ODM kinawataka wabunge Aisha Jumwa wa Malindi na Suleimani Dori kufika mbele ya kamati ya nidhamu ya chama hicho kufikia tehe 10 mwezi ujao.Wawili hao pamoja na wanasiasa wengine 8 watatakiwa kujieleza ni kwanini hawafai kuadhibiwa kwa kukiuka misimamo ya chama.Juma na Dori ni miongoni mwa wanasiasa wa ODM ambao mapema mwaka huu walitangaza kumuunga mkono naibu wa rais William Ruto katika azma yake ya kuwania urais.Wengine waliotakiwa kufika mbele ya kamati hiyo ya nidhamu ni pamoja na waakilishi wadi 6 wa kaunti ya Nyamira,kiongozi wa wachache kaunti ya Nakuru na mwakilisi mmoja wa kaunti ya Busia.

Show More

Related Articles