HabariMilele FmSwahili

Mkewe gavana Obado aagizwa kufika katika makao ya DCI Migori

Mkewe gavana wa Migori Okoth Obado Hellen Obado ameagizwa kufika katika makao ya DCI katika kituo cha polisi cha Migori kuhojiwa kuhusiana na mauaji ya Sharon Otieno aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo.  Haya yanajiri huku polisi wakitaka kujua iwapo alihusika kivyovyote katika  mauaji hayo hasaa baada ya gavana Obado kukiri kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Sharon. Wakati uo huo dereva wa gari lililotumika kumteka nyara Sharon kabla ya kuwawa anafikishwa katika mahakama ya Kisii wakati wowote kuanzia sasa.

Show More

Related Articles