HabariMilele FmSwahili

Baadhi ya wenyeji wa Nairobi waandamana nje ya hospitali ya Pumwani

Baadhi ya wenyeji kaunti ya Nairobi wanaandamana wakati huu nje ya hospitali ya kujifungua kinamama ya Pumwani. Waandamanaji hao wanalalamikia kisa cha miili ya watoto 12 kupatikana katika mifuko ya plastiki hospitalini humo. Yakijiri hayo  gavana wa Nairobi anatarajiwa hospitalini humo asubuhi hii. Tayari Sonko amewasimamisha kazi, katibu wa kaunti Peter Kariuki, afisa mkuu wa afya Mahat Jimale, mkuu wa kaunti Lydia Kwamboka kutokana na msimamo waliotoa kinzani kuhusu hali halisi katika hospitali hiyo. Katika taarifa Sonko amemteuwa Pauline Kahiga kuwa kaimu katibu wa kaunti, Charles Kerich kuwa kaimu waziri wa afya Nairobi na Mohamed Saleh kuwa kaimu afisa mkuu wa afya Nairobi

Show More

Related Articles