HabariSwahili

Licha ya kujipiga kifua, wabunge wa Jubilee na NASA watii vinara wao

Ni wazi sasa kwamba kinara wa ODM Raila Odinga alihusika pakubwa katika kuwashawishi wabunge wa chama hicho kuunga mkono mapendekezo ya rais kwenye mswada wa fedha uliorejeshwa bungeni.
Baadhi ya viongozi wa chama cha ODM akiwemo kiongozi wa wachache John Mbadi walikuwa wameahidi kupinga mapendekezo ya rais lakini hii leo hawakuwa na budi ila kutii agizo la kinara wao.
Anders Ihachi alihudhuria kikao cha ODM kilichoongozwa na Raila Odinga na amezungumza pia na kiongozi wa wengi kwenye bunge la kitaifa Aden Duale kutathmini ni vipi mkondo wa mambo uligeuka ghafla bin vuu.

Show More

Related Articles