HabariSwahili

Baadhi ya shule Tana River, Kilifi hazijarejelea masomo kufuatia gharika 

Baada ya mafuriko yaliyoathiri maeneo ya Kilifi, mamia ya watu walipoteza makao, lakini walioathirika zaidi, ni wanafunzi katika shule zilizoko kando kando mwa mto Galana na Sabaki
Shule moja iliyoko Magharini ambayo kando na kufunikwa kabisa kwa maji ya mafuriko, madawati, vyakula na vitabu vya wanafunzi na walimu vilisombwa.
Miezi minne baadaye, shule hii, kwa sasa, imejimudu kupata madawati kwa wanafunzi wa darasa la saba na la nane.
Wengine wote, wanafunzi 430, wanaketi sakafuni wakisoma anavyoarifu Dennis Matara.

Show More

Related Articles