HabariSwahili

Kiinimacha cha Pumwani : Serikali ya kaunti ya Nairobi yakiri haijawajibikia mtafaruku uliopo

Siku moja tu baada ya gavana wa Nairobi Mike Sonko kuzuru hospitali ya kujifungua kina mama ya Pumwani na kuzua kioja kuhusu maiti za watoto zilizodaiwa kufichwa zikiwa kwenye mifuko ya plastiki,sasa inaonekana kwamba serikali ya kaunti imekiri kutowajibikia majukumu yake.
Swali ni je,nini kilichomchochea gavana Sonko kufika ghafla hospitali humo na kuivunjilia mbali bodi ya hospitali hiyo na pia kuwasimamisha kazi baadhi ya wasimamizi ilihali imebainika kuwa serikali ya kaunti haijawajibikia majukumu yake kiafya?

Show More

Related Articles