HabariMilele FmSwahili

Wabunge wa ODM waunga mkono pendekezo la rais kupunguza ushuru kwa mafuta

Wabunge wa chama cha ODM wameunga mkono pendekezo la rais Uhuru Kenyatta kupunguza ushuru wa bidhaa za mafuta kutoka asilimia 16 hadi asilimia 8.Kiranja wa wachache bungeni Junet Mohammed anasema baada ya mkao wa saa 2 chini ya uongozi wa Raila Odinga wameafikiana kumuunga mkono rais japo kwa muda wa mwaka mmoja.Kadhalika wanataka pia kusitishwa kwa matumizi yasiofaa kwa watumishi wa umma ili kuhifadhi fedha

Show More

Related Articles