HabariMilele FmSwahili

KMPDU yakosoa hatua ya Sonko kuwasimamisha kazi wakuu 3 wa hospitali ya Pumwani

Chama cha madaktari nchini KMPDU kimekosoa hatua ya gavana wa Nairobi Mike Sonko kuwasimamisha kazi wakuu watatu wa hospitali ya kujifungua kina mama ya Pumwani.Katika ujumbe kupitia mtandao wa Twitter, katibu mkuu wa KMPDU Dkt Ouma Oluga anasema changamoto zinazokumba hospitali hiyo zinapaswa kutatuliwa kwa njia ya ustaarabu. Dkt Oluga anapendekeza hospitali ya Pumwani kupandishwa hadhi kuwa na rufaa na kusimamiwa na serikali kuu badala ya kaunti ta Nairobi.  Naye kaimu mkurugenzi wa afya kaunti ya Nairobi, Dkt Lucina Koyoo amedhibitisha miili 11 hiyo imepelekekwa kuhifadiwa. Amekiri kuwepo utepetevu katika hospitali hiyo hasaa kuhusu shughuli ya kuondoa na kusafirisha miili ya watoto wanaofariki hospitalini humo

Show More

Related Articles