HabariMilele FmSwahili

Wabunge wa Jubilee na ODM kushiriki mikao maalum na vinara wao

Wabunge wa Jubilee na wale wa ODM wanatarajiwa kuanza kuwasili katika ikulu na jumba la Orange wakati wowote kuanzia sasa 10 kushiriki mikao maalum na vinara wao.Mikao hiyo inalenga kujadiliana kuhusu hatima ya mapendekezo ya rais Uhuru Kenyatta kutaka kupunguzwa ushuru wa bidhaa za mafuta kutoka asilimia 16 hadi 8. Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto wanatarajiwa kuwashawishi wana Jubilee kuunga mkono mapendekezo hayo ambayo wengi wameapa kuyapinga wakidai yatawaumiza wakenya.Kiranja wa wengi bungeni Ben Washiali ametoa onyo kali kwa watakaosusia mkao na vinara hao akisema wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria za bunge.Katika jumba la Orange,kiongozi wa wachache John mbadi anatarajiwa kuongoza mkao wa wanachungwa ambao wengi wameapa kupinga mapendekezo ya rais Uhuru Kenyatta wakisema wanachotaka ni ushuru wa bidhaa za mafuta kuondolewa kabisa.

Show More

Related Articles