HabariMilele FmSwahili

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Multi Media Nairobi waandamana

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Multi Media Nairobi wamegoma leo na kuandamana katika bara bara ya Magadi.Wanafunzi hao waliofunga kwa muda bara bara hiyo na kutatiza uchukuzi wanasema usimamizi wa chuo umefeli kutatua suala la uhaba wa mabweni chuoni humo. Suala la gharama ya juu ya vyakula chuoni humo pia limejitokeza. Baadhi ya wanafunzi wanadaiwa kuelekea hadi mjini Rongai ambapo wamekabiliana kwa muda na baadhi ya wakazi.

Show More

Related Articles