HabariMilele FmSwahili

Elachi kubaini hatma yake leo kuhusiana na kesi ya kuzuia kubanduliwa mamlakani

Spika wa bunge la kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi atabaini hatma yake hivi leo akifika mbele ya jaji Maureen Onyango kupata mwelekeo kuhusiana kesi yake ya kuzuia kubanduliwa mamlakani na wawakilishi wadi kaunti ya Nairobi. Elachi anadai wawakilishi hao hawakumpa muda wa kujitetea kabla ya kupasisha kura kumuondoa, hivyo walichukua hatua hiyo kinyume na sheria. Wawakilishi wadi wanaoshinikiza kumtimua Elachi nao wanatarajiwa kufika mbele ya tume ya maadili na kupambana na ufisadi.Wamesimama kidete kuwa hawatakubali hatua hayo kubatilishwa kupitia tume hiyo au mahakama.

Show More

Related Articles