HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta atangaza kupunguzwa ushuru wa mafuta

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kupunguzwa ushuru wa mafuta kutoka asilimia 16 hadi asilimia 8.Amewataka wabunge kuangazia tena mswaada wa fedha ili kufanikisha utendakazi wa serikali.Amekiri mswaada huo ulikosa kuangazia maslahi ya wakenya.Hata hivyo anasema bado kuna upungufu kwenye ufadhili wa miradi ya serikali akitangaza mikakati kadhaa ikiwemo kupunguzwa matumizi ya safari za ndani na nje ya nchi sawa na mafunzo kwa wafanyikazi kuelekezwa fedha hizo kwingine.na ili kulinda ushuru wa wananchi, ameongeza bajeti ya idara ya mahakama, asasi za kupambana na ufisadi pamoja na afisi ya mkuu wa mashtakata ya umma kukabili wafisadi.

Show More

Related Articles