HabariMilele FmSwahili

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Cooperative apatikana amejiua Kericho

Uchunguzi umeanzishwa kufuatia kisa ambapo mwanafunzi wa chuo kikuu cha Cooperative kaunti ya Kericho anayedaiwa kujiua kwenye hoteli moja eneo la Kapsoit, kaunti ndogo ya Ainamoi. OCPD Phillip Okello anasema marehemu aliyekuwa mwanafunzi wa chuo cha Cooperative jijini Nairobi, aliwapigia simu jamaa zake kuwaeleza nia ya kufanya hivyo. Okello aidha amebaini kuwa dawa fulani inayoaminika kutumiwa na marehemu kujitoa uhali ilipatikana kando ya kitanda. Mwili wa marehemu, aliyekuwa na umri wa miaka 21 umepelekwa kwenye chumba cha maiti cha hospitali ya rufaa ya kaunti ya Kericho.

Show More

Related Articles