HabariMilele FmSwahili

Serikali kuwalipa wakulima waliowasilisha mahindi kwa NCPB wiki ijayo

Serikali itawalipa wiki ijayo wakulima waliowasilisha mahindi kwa bodi ya mazao na nafaka NCPB. Waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa ametoa hakikisho huku akisema zoezi la ukaguzi wa wanaopaswa kulipwa tayari limekamilika. Wakulima hao wamekuwa wakisubiri malipo yao tokea Oktoba mwaka jana na Machi mwaka huu. Mapema mwezi huu serikali ilipa shilingi bilioni 1.4 kati ya bilioni 3.5 ilizokuwa ikidaiwa na wakulima.

Show More

Related Articles