HabariMilele FmSwahili

Vitengo vya polisi wa kawaida na polisi wa utawala vyajumuishwa kuwa kitengo 1

Vitengo vya polisi wa kawaida na polisi wa utawala vimejumuishwa na sasa kitakuwa kitengo kimoja moja cha polisi wa kutoa huduma kwa wote. Rais Uhuru Kenyatta ametangaza mabadiliko ambayo anasema polisi wa kawaida 39,680 watajumuishwa na wenzao wa utalawa 24,572  kuimarisha utendakazi na kupunguza matumizi ya fedha uliokuwepo kutokana na  vitengo vingi vinavyotekeleza jukumu sawa akizungumza kwa mara ya kwanza tangu alipotoka Uchina, ameagiza naibu inspekta wa polisi wa kawaida kusimamia usalama wa raia na ulinzi wa taifa huku naibu inspekta mkuu anayesimamia polisi wa utawala kusimamia ulizi wa mipaka na kukabili wizi wa mifugo.

Show More

Related Articles