HabariMilele FmSwahili

Rais atangaza mabadiliko ya uongozi katika idara ya polisi

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza mabadiliko ya uongozi katika idara ya polisi yatakayotekelezwa kuanzia Disemba mwaka huu.Rais Kenyattta ameagiza naibu inspekta wa polisi wa kawaida kusimamia masuala ya usalama wa raia na ulinzi wa taifa. Aidha naibu inspekta mkuu anayesimamia polisi wa utawala sasa atatwikwa wajibu wa kusimamia ulizi wa mipaka na kukabili wizi wa mifugo.Akihutubu katika mkutano wa  maafisa wakuu wa usalama uliondaliwa hapa jijini rais pia ametangaza kuwa idara ya polisi itakuwa na magwanda mapya ya rangi ya samawati.Vile vile rais Kenyatta amesema kuwa maafisa wa polisi sasa wataanza kopokea marupu rupu ya nyumba katika hatua inayonuiwa kutatua suala na makaazi duni ya polisi

Show More

Related Articles