Mediamax Network Limited

Gavana wa Migori ajiondolea lawama kuhusu mauaji ya kikatili

Gavana wa Migori Okoth Obado amekanusha madai ya kuhusika kwa njia yeyote ile katika mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno .

Japo amekataa katakata kuzungumzia uhusiano wake na Sharon, Obado amewashtumu wanasiasa kwa kumhusisha na mauaji hayo ,na kusisitiza  kuwa maafisa wa polisi wafanye kila juhudi kuwanasa wauaji wa Sharon.