HabariMilele FmSwahili

Matiang’i kuweka wazi ripoti ya mageuzi katika idara ya polisi hapo kesho

Waziri wa usalama wa taifa dakta Fred Matiangi anasema wataweka wazi ripoti ya mageuzi yanaofanyiwa idara ya polisi hapo kesho.Ni ripoti ambayo inatarajwia kuangazia miongoni mwa masuala mengine pendekezo la kujumuisha polisi wa utawala na wale kawaida.  Akizungumza katika mkutano na maafisa wa usalama hapa Nairobi,Matiangi amewaondolea hofu maafisa hao na kuwahakikishia mageuzi hayo yatasaidia kuanisha utendakazi wa idara ya polisi.Ameongeza mageuzi hayo pia yatafanikisha zaidi utoaji usalama na kuangazia maslahi ya maafisa wa usalama.

Show More

Related Articles