HabariPilipili FmPilipili FM News

Shughli Za Usafiri Zatatizika Katika Kuvukio Cha Ferry Cha Likoni.

Huduma za usafiri katika kivuko cha Likoni ferry zimetatizika mapema hii leo baada ya ferry mpya ya MV JAMBO kushuhudia hitilafu za kimitambo.
Ferry hiyo ambayo ilikwama mahali pa kuegeshea ilisababisha msongamano mkubwa wa magari na abiria.
Kwa sasa imeweza kuondolewa huku Ferry zilizisalia  zikihudumia abiria.

Wakati uo huo wananchi wamezidi kuilamu serikali ya kitaifa kwa kushindwa kudhibiti tatizo la usafiri katika kivuko cha Likoni wakihoji kuwa shughuli zao za kila siku zimekuwa zikilemazwa huku uchumi wa kaunti ukiathirika.

Kufikia sasa huduma kwenye kivuko hicho zinaendelea japo kwa polepole huku msongamano wa magari ukizidi kushuhudiwa.
Kupitia mtandao wa twitter shirika la KFS limeomba radhi kufuatia hali hiyo.

Show More

Related Articles