Mediamax Network Limited

Wizara ya fedha yanuia kukusanya shilingi bilioni 35 kufuatia nyongeza ya ushuru kwa mafuta

Wizara ya fedha sasa inasema inanuia kukusanya shilingi bilioni 35 kufuatia nyongeza ya ushuru wa bidhaa za mafuta. Akihojiwa na kamati ya bunge ya kawi naibu waziri wa  fedha Nelson Gaichuhie amekanusha madai kuwa serikali inakusudia kukusanya ushuru wa shilingi bilioni 70. Kadhalika amekana madai kuwa serikali inakabiliwa na shinikizo kutoka kwa shirika la fedha ulimwenguni IMF kuongeza ushuru huo. Amesema tume ya kawi ERC na ile ya kukusanya ushuru KRA zinatekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria ya ushuru wa VAT ya 2013. Hata hivyo amedokeza kuwa rais Uhuru Kenyatta na waziri wa fedha Henry Rotich wanakutana leo kuangazia utata wa ushuru huo.