Mediamax Network Limited

Hospitali Ya Makadara Yalaumiwa Kwa Kutowashughulikia Wagonjwa Ipasavyo.

Imebainika kuwa msichana wa darasa la 6 aliyevamiwa na kujeruhiwa na wahalifu na kisha kulazwa katika hospitali ya makadara hapa mombasa hashughulikiwi inavyostahili.

Imebainika pia msichana huyo hapewi matibabu licha ya  hospitali hiyo kuwa ya umma ambapo hakupaswa kulipa chochote.

Akizunguza na meza yetu ya habari Roma Juma mmoja wa jamaa za familia ameitaka serikali iingilie kati ili msichana huyo aweze kutibiwa ,kwani anaweza kuwa na usaidizi mkubwa katika kutoa taarifa kuhusu wahalifu waliomvamia na kumjeruhi vibaya.