Mediamax Network Limited

Mshukia Wa Mauaji Ya Sharon Otieno Atazidi Kuzuiliwa Korokoroni.

Mshukiwa wa mauaji ya mwanafunzi Sharon Otieno Oyamo Oyacho ataendelea kuzuiliwa kwa muda wa siku 14 zaidi ili upande wa mashtaka kukamilisha uchunguzi wake.

Agizo hilo limetolewa na jaji wa mahakama kuu Luka Kimaru ambapo sasa atafikishwa tena mahakamani tarehe 26 ya mwezi huu.

Hii ni baada ya upande wa mashtaka kuitaka mahakama hiyo kuruhusu polisi kumzuia kwa siku 14 zaidi.

Mawakili wa upande wa mashtaka ameiambia mahakama  kuwa polisi wananuia kumfanyia Oyamo uchunguzi wa kiakili na kuchukua chembechembe zake za DNA.

Awali mawakili wa Oyamo waliitaka mahakama kutupilia mbali ombi hilo wakidai polisi wamekuwa na muda wa kutosha kukusanya ushahidi tangu walipomkamata Oyamo wiki iliyopita.