Mediamax Network Limited

Rais ahimizwa kuitisha kikao kusaka mwafaka kuhusiana na ushuru unaotozwa mafuta

Katibu mkuu wa muungano wa COTU Francis Atwoli sasa anamtaka rais Uhuru Kenyatta kuitisha kikao cha dharura cha wadau mbali mbali kusaka mwafaka kuhusiana na ushuru wa asilimia 16 unaotozwa bidhaa za mafuta. Atwoli amesema ni jambo la kutamausha kwa rais kutozungumzia suala hilo siku mbili baada ya kurejea nchini. Ameelezea haja ya suluhu ya upesi kupatikana ili kumwokoa mwananchi dhidi ya kupanda gharama ya maisha.