HabariMilele FmSwahili

Upande wa mashtaka waitaka mahakama kumzuia kwa siku zaidi ya 14 Oyamo

Upande wa mashtaka unaitaka mahakama ya milimani kuruhusu polisi kumzuia kwa siku 14 zaidi Micheal Oyamo mshukiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno. Mawakili wa upande wa mashtaka wamemwambia jaji Luka Kimaru kuwa polisi wananuia kumfanyia Oyamo uchunguzi wa kiakili na kuchukua chembechembe zake za DNA. Hata hivyo mawakili wa Oyamo June Ashioya na Rodgers Abisai wanaitaka mahakama kutupilia mbali ombi hilo wakidai polisi wamekuwa na muda wa kutosha kukusanya ushahidi tangu walipomkamata Oyamo wiki iliyopita.

Show More

Related Articles