HabariMilele FmSwahili

Mahakama yaongeza muda wa kuzuia kumbandua Elachi mamlakani

Mahakama ya leba imeongeza muda wa kuzuia utekelezwaji wa hatua  ya kumbandua mamlakani spika wa bunge la kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi. Jaji Stephen Riech ameagiza kuwa Elachi atasalia mamlakani hadi septemba 14 ambapo ataamua iwapo mchakato wa kumbandua afisi ulifuata sheria au la. Hii ni baada ya Elachi kupitia wakili Harrison Kinyanjui kuitaka mahakama kuwapata wawakilishi wadi na hatia ya kupuuza agizo la hapo awali la kusitisha mchakato huo. Hata hivyo wakili wa bunge la kaunti ya Nairobi Tom Ojienda amepinga ombi la Elachi akisema kura ya zoezi la kumwondoa lilianza kabla yake kupata agizo la mahakama kulizuia.Yakijiri hayo afisi ya spika wa bunge la kaunti ya Nairobi imesalia wazi leo baada ya spika Beatrice Elachi kukosa kufika afisini. Aidha kadhalika wawakilishi wadi waliomfurusha Elachi afisini jana leo wanakongamana katika eneo la siri nje ya jijini katika mkutano unaotajwa kuwa wa kupanga mkakati wa kumteua aliyekuwa spika Alex Ole Oagelo kutwaa wadhifa wa Elachi.

Show More

Related Articles